SiasaSyria
Syria yakabiliwa na kesi katika Mahakama ya ICJ
12 Juni 2023Matangazo
ICJ yenye makao yake mjini The Hague imesema nchi hizo zinaishutumu Damascus kwa kukiuka mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya mateso au ukatili mwingine, ikiwa ni pamoja na matumizi ya silaha za kemikali.
Uholanzi na Canada zaitaka ICJ kuchukuwa hatua za haraka dhidi ya Syria
Uholanzi na Canada zimeitaka Mahakama ya ICJ kuchukua hatua za haraka, ikiwa ni pamoja na kuiamuru Syria kuwaachia huru wafungwa ambao wamezuiliwa kiholela. Hii ni mara ya kwanza kwa Syria kufikishwa Mahakamani kufuatia vita hivyo vilivyozuka mnamo mwaka 2011 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 500,000.