1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapinduzi yaliokwapuliwa Syria

15 Machi 2017

Katika sehemu nyingi za  Ulimwengu wakiarabu, vuguvugu la mabadiliko la 2011 kwa muda mrefu limeacha hali ya kukata tamaa. Nchini misri anayedhibiti  hatamu za utawala ni Jenerali Sisi,

https://p.dw.com/p/2ZDkG
Syrien Zerstörung
Wanawake wanatembea karibu na jengo lililoporomoka katika mji wa al-Bab, kaskazini mwa SyriaPicha: Reuters/K. Ashawi

Huko Bahrain familia ya Al-khalifa bado inatawala. Nchini Libya  baada ya kun´golewa madarakani Gaddafi nchi hiyo imeingia katika machafuko. Lakini yote hayo yamegubikwa na hali ya mambo nchini Syria. Kile kilichoanza kama maandamano ya amani Machi 2011 sasa kimepamba moto na kugeuka vita vya kikatili ambavyo vimedumu muda mrefu kuliko vita vya pili vya dunia.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa hivi sasa zaidi ya watu 400,000 wamegeuka wahanga wa vita hivyo. Mgogoro huo umesababisha wimbi kubwa la wakimbizi la wakati huu. Zaidi ya nusu ya wakaazi wapatao milioni 21 wa Syria wameyakimbia makaazi yao.

Mjini Geneva, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za binadamu Seid raad al-Hussein amesema wiki hii kwamba mzozo wa Syria ni janga kubwa kabisa la binaadamu tangu vita vya pili vya dunia. Nchi hiyo imegeuka kuwa  ukumbi wa mateso.

Mauwaji dhidi ya raia

Mtawala Bashar al-Assad kama alivyokuwa baba yake Hafidh al-Assad  analitumia jeshi kuwashambulia na kuwauwa raia wake mwenyewe kwa mabomu au kama asemavyo mtaalamu kuhusu Syria katika  taasisi ya  Carnegie  inayohusika na Mashariki ya kati Yezid Sayigh, " baba na mtoto wamedhihirisha nia zao katika kutumia  nguvu kupita kiasi.”

Mtazamo usiowa kawaida wa hali nchini Syria ulifafanuliwa na Makamu wa zamani wa rais wa Marekani Joe Biden katika mhadhara kwa wanafunzi wa Chuo kikuu cha Harvard Oktoba  2, mwaka  2014. Wakati wa maswali na majibu kwenye mhadhara huo wa dakika 52, Biden alisema, " Washirka wetu  ndiyo tatizo letu kubwa nchini Syria. Uturuki, Saudi Arabia na  Umoja wa Falme za Kiarabu-wote lengo lao kubwa likuwa ni kumuangusha Assad na kusababisha vita baina ya Wasunni na Washia  huku zikimimina mamilioni ya dola na tani elfu kadhaa za silaha kwa kila mmoja wao-Al Nusra na Al-Qaeda pamoja na wapiganaji wa jihadi wa siasa kali kutoka kote duniani.” Biden akawaambia wanafunzi hao, "Msikate tama katika kuisaidia Syria.

Jitihada zilizoshindwa nchini Syria

Syrien Interview Bashar al-Assad mit französischen Journalisten in Damaskus
Rais Bashar al-Assad wa SyriaPicha: Reuters/Sana

Lakini kile ambacho Biden hakukisema ni kwamba  mpango wa muda mrefu wa Marekani yenyewe  kutaka kuleta mabadiliko ya utawala Syria, hata kabla ya mwaka 2011 haukufanya kazi. Kwa mfano ni ujumbe  wa shughuli za ubalozi wa Marekani mjini Damascus uliochapishwa na mtandao wa Wikileaks  na kufichuwa kwamba  afisa wa ubalozi wa marekani mjini Damascus William Roebuck alitamka  mnamo Desemba 2006 kwamba   wanaamini udhaifu wa  Bashar uangaliwe  kwa namna anavyochukua hatua  wakati wa hatari, kwa mfano  kwa kupima mgongano uliopo kati ya  mageuzi ya kiuchumi na kitisho kikubwa kwa utawala wake kutokana na  kuongezeka kwa idadi ya wafuasi wa itikadi kali. Katika ujumbe huo huo afisa huyo wa Marekani akapendekeza  upaliliwe mzozo kati ya Wasunni na Washia.

Kwa upande  mwengine baada ya miaka sita ya vita,  Urusi na Iran ndiyo nguvu kubwa nchini Syria. Kwa wanaowaunga mkono wapinzani, mtaalamu Sayigh anasema, Marekani, nchi za Ulaya, Saudi Arabia na Qatar na pia Uturuki tangu katikati ya mwaka jana wanachukua msimamo. Lakini mtaalamu huyo anasema pamoja na kuwa wamejaribu kumaliza vita hivyo, lakini yeye binafsi hatarajii kutapatikana makubaliano rasmi, badala yake utawala wa Assad utaendelea kuweko madarakani.

Huo ni mtazamo wa wachambuzi wengi  barani Ulaya. Hata ikiwa vita vitaendelea kwa miaka michache, swali la ujenzi mpya wa Syria ambayo imeharibiwa kwa sehemu kubwa litakuwa zingatio kubwa Na ndiyo maana kuna haja ya  uumoja wa Ulaya kujihusisha zaidi katika kutafuta suluhisho, kwani kwa jumla kwa Wasyria  unazingatiwa kuwa ni mshirika wa kuaminika   sio tu nchini Syria kanda  nzima ya Mashariki ya kati. Mchango wa Ulaya usiwe tu katika  misaada ya kiutu bali  suluhisho la kisiasa. Hilo litakuwa jambo jema kwasababu tatizo la Syria liko moja kwa moja, mlangoni mwa Ulaya.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman / von Hein, Matthias, dw
Mhariri: Yusuf Saumu