Kwa mujibu wa takwimu, thuluthi moja ya wanafunzi nchini Ujerumani wamo katika hati hati ya kukumbwa na umasikini. Kutokana na kupanda kwa bei za nishati baadhi ya wanafunzi wameamua kuacha kujipikia chakula wenyewe. Asasi inayoshugulikia ustawi wa jamii imesema Ujerumani imo miongoni mwa mataifa tajiri duniani lakini wapo watu milioni 13.8 wanaohesabika kuwa maskini. Mtayarishaji ni Zainab Aziz.