Sunak akutana na Macron mjini Paris
10 Machi 2023Matangazo
Mkutano huo unalenga kuzungumzia mvutano wa miaka mingi kuhusu Brexit na mkataba mpya wa wahamiaji wanaotumia ujia wa bahari unaoitenganisha Uingereza na Ufaransa.
Sunak alipongeza uhusiano kati ya nchi hizo, kabla ya mkutano huo, ambako viongozi hao wanatarajia pia kuahidi msaada kwa Ukraine na usalama katika eneo la Asia-Pasifiki. Macron alimkaribisha Sunak katika Ikulu ya Ufaransa Elysee, baada ya kuwasili Paris kwa treni.
Huo ni mkutano wa kwanza kati ya Uingereza na Ufaransa kufanyika katika kipindi cha miaka mitano, baada ya Sunak kuwa waziri mkuu Oktoba, mwaka 2022.