1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaOman

Sultani wa Oman anafanya ziara nchini Iran

28 Mei 2023

Sultani wa Oman Haitham bin Tariq al-Said amewasili nchini Iran leo kwa ziara ya siku mbili inayotarajiwa kutuama juu ya masuala ya usalama na diplomasia ya kikanda.

https://p.dw.com/p/4Rv0H
Sultan wa Oman Haitham al-Said akiwasili mjini Tehran
Sultan wa Oman Haitham al-Said akiwasili mjini Tehran Picha: Hamed Jafarnejad/Fars

Sultan al-Said alilakiwa na makamu wa rais Mohammad Mokhber kwenye uwanja wa ndege wa Mehrabad mjini Tehran na baadaye alikutana kwa mazungumzo na rais Ebrahim Raisi katika kasri la Sadabad kaskazini wma Tehran. 

Ziara yake inafanyika ikiwa ni siku mbili tangu Oman ilipofanikisha mazungumzo ya kubadilishana wafungwa kati ya Iran na Ubelgiji. Oman imekuwa mpatanishi wa muda mrefu kati ya Iran na mataifa ya magharibi kupitia mazungumzo yaliyofanikisha kuachiwa kwa raia kadhaa wa kigeni.

Sultani al-Said anaitembelea Tehrani wakati ukosoaji unaongezeka kuhusiana na rikodi dhaifu ya haki za binadamu nchini Iran na madai kuwa dola hiyo ya uajemi inaipatia silaha Urusi kupigana vita nchini Ukraine.