1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSudan

Sudan yapinga ripoti kuhusu njaa inayoungwa mkono na UN

29 Desemba 2024

Serikali ya Sudan imepinga ripoti iliyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa iliyosema kwamba njaa imeenea katika maeneo matano yanayozongwa na machafuko nchini humo.

https://p.dw.com/p/4ofQX
Machafuko ya Sudan
Jenerali Abdel-Fattah Burhan, mkuu wa majeshi ya SudanPicha: Marwan Ali/AP/dpa/picture alliance

Kulingana na ripoti iliyotolewa wiki iliyopita, vita kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF vimesababisha hali ya njaa kwa watu 638,000, huku wengine milioni 8.1 wakiwa katika hatari ya kukumbwa na viwango vya kutisha vya njaa.

Kupitia taarifa, wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imesema jeshi la nchi hiyo limepinga moja kwa moja ripoti hiyo ya shirika la IPC.

Taarifa imeitaja ripoti hiyo kuwa ya utabiri huku ikiishutumu kwa kujaa mapungufu ya uwazi na utaratibu.

Wizara hiyo imesema waandaaji wa ripoti hawakujumuisha data iliyosahihishwa ya hali ilivyo mashambani na hawakushauriana na timu ya kiufundi ya serikali kabla ya kuchapisha ripoti hiyo.