Sudan yamjia juu balozi wa Ethiopia juu ya ndege iliyoanguka
31 Agosti 2022Matangazo
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Khartoum Jumatatu asubuhi kuhusu wimbi jipya la mapigano kaskazini mwa Ethiopia, Balozi Yibeltal Aemero Alemu alisema hakuna shaka lolote juu ya mahali ilipotokea ndege hiyo.
Wizara ya mambo ya nje ya Sudan amesema kuwa mkurugenzi mkuu wa masuala ya Afrika Fadl Abdallah Fadl aliitaja taarifa ya balozi wa Ethiopia kuwa tuhuma zisizo na msingi, na ukiukaji wa taratibu za kidiplomasia, hususan inapohusika nchi jirani inayotaka kuimarisha mahusiano.
Wiki iliyopita, jeshi la anga la Ethiopia lilisema limeiangusha ndege iliyokuwa ikiwapelekea silaha waasi wa kundi la Ukombozi wa Watu wa Tigray, TPLF, baada ya ndege hiyo kuingia katika anga ya Ethiopia ikitokea Sudan.