Sudan Kusini yapuuza ripoti ya ufisadi ya UN
28 Septemba 2021Matangazo
Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini ilionya wiki iliyopita kwamba uporaji huo una hatari ya kuharibu mchakato wa amani.
Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa imesema kwamba dola milioni 73 ni sehemu tu ya fedha jumla zilizoporwa, na kuongeza kuwa Rais Salva Kiir aliwahi kukiri tangu mwaka 2012 kwamba wanasiasa wa Sudan Kusini wamechota zaidi ya dola bilioni nne.
Hata hivyo Sudan Kuisni imekana shutuma hizo na kiongozi wa baraza la mawaziri, Martin Elia Lomuro, amesema ripoti hiyo ni sehemu ya kile alichokiita "kampeni ya kimataifa dhidi ya serikali yake".