1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan Kusini

Sudan Kusini yaongeza matumizi yake katika bajeti

20 Juni 2023

Sudan Kusini inapanga kutumia paundi trilioni 2.1 katika mwaka wa fedha unaoanza mwezi ujao.

https://p.dw.com/p/4SqeH
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini, Salva KiirPicha: Samir Bol/ZUMAPRESS/picture alliance

Sudan Kusini inapanga kutumia paundi trilioni 2.1 katika mwaka wa fedha unaoanza mwezi ujao.

Waziri wa fedha wa Sudan Kusini Dier Tong Ngor amesema kiwango hicho ni asilimia 33 zaidi ikilinganishwa na bajeti ya mwaka uliopita.

Akiiwasilisha bajeti kwa wabunge hivi leo waziri Ngor amesema matumizi yataelekezwa katika kuchochea ukuaji uchumi kupitia hatua za mageuzi katika nakisi, fedha na muundo.

Hata hivyo hakufafanua kuhusu hatua hizo wala kutoa makadirio ya ukuaji uchumi kwa mwaka wa fedha unaokuja.

Waziri Ngor amesema ili kuidhamini bajeti kiasi cha paundi bilioni 1.8 za Sudan Kusini zitatafutwa ndani ya nchi, ikiwemo kupitia mapato ya mafuta, huku fedha nyingine zikitafutwa kupitia kuomba mikopo.