1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Sudan inatumbukia katika majanga ya uharibifu na uharibifu

19 Juni 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema hii leo kuwa Sudan inadidimia kwenye majanga ya vifo na uharibifu mkubwa, kwa kasi ambayo haijawahi kushuhudiwa.

https://p.dw.com/p/4Slyb
Sudan Khartum | Rauch und Flammen in Omdurman
Picha: REUTERS

Guterres ameyasema hayo leo mjini Geneva katika mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa, akiwataka wafadhili kuingilia kati na kuzuia maafa yanayoendelea. Hadi sasa wito wa kuisaidia Sudan umefadhiliwa kwa karibu asilimia 17 pekee.

Umoja wa Mataifa umesema unahitaji kiasi dola bilioni 3 kufadhili shughuli zote za kibinaadamu nchini Sudan mwaka huu lakini pia kushughulikia tatizo la wakimbizi wa nchi hiyo walioko katika mataifa jirani.

Mpango huu wa kukusanya msaada kwa Sudan unaratibiwa kwa pamoja na mashirika yanayohusika na masuala ya kibinadamu na wakimbizi ya Umoja wa Mataifa pamoja na Misri, Ujerumani, Qatar, Saudi Arabia, Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya.

AFP