1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Stoltenberg asema anataraji msaada wa kutosha kwa Ukraine

10 Julai 2024

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg amesema anatumai viongozi wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo wataidhinisha msaada wa kutosha kuipiga jeki Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4i7TS
USA Washington 2024 | Katibu Mkuu wa NATO Stoltenberg katika hafla ya kuadhimisha miaka 75 ya muungano huo
Katibu Mkuu Jens Stoltenberg akizungumza wakati wa hafla ya kusherehekea miaka 75 ya NATO kwenye Ukumbi wa Andrew Mellon Julai 9, 2024 huko Washington, DC.Picha: Andrew Harnik/Getty Images

Stoltenberg alikuwa akizungumza na waandishi habari muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya NATO unaofanyika mjini Washington ambao kwa mara nyingine unakubikwa na kiwingu cha vita vya Ukraine.

"Tutafanya pia maamuzi muhimu kwa ajili ya siku zijazo: kuhusu yale yanayoendelea Ukraine na jinsi ya kutanua maingiliano yetu hususani na washirika wetu wa kanda ya Asia na Pasifiki. Kuhusu Ukraine, ninataji washirika watakubaliana kiwango cha msaada wa kukidhi mahitaji".
Soma pia:Viongozi wa NATO kutangaza msaada kwa Ukraine

Katika hatua nyingine Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken ametangaza kuwa washirika wa NATO tayari wameanza kuipelekea Ukraine, ndege mamboleo za kivita chapa F-16 kuisaidia kuimarisha ulinzi wake wa anga.

Amesema ndege kutoka Denmark na Uholanzi ziko njiani kwenda Ukraine.