1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

STOCKHOLM : Waustralia wawili washinda tuzo ya Nobel ya madawa

3 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEVB

Wananchi wawili wa Waustralia wamejishindia tuzo ya Nobel ya madawa leo hii kwa kugunduwa kijibakteria kinachosababisha mwako na vidonda vya tumbo ugonjwa ambao huwaathiri mamilioni ya watu na kuupatia makampuni ya madawa mabilioni ya dola.

Baraza la Nobel mjini Sockholm ambayo ni Taasisi ya Karolinska imesema inawatunukia crown milioni 10 fedha za Sweden sawa na dola milioni moja na laki 29 Barry Marshall na Robin Warren kwamba kuvunja imani iliojikita kwamba vidonda vya matumbo husababishwa na mtindo wa maisha pamoja na dhiki.

Watafiti hao wa tiba walifanya ugunduzi huo mkubwa wa kupigiwa mfano hapo mwaka 1982 kwamba ugonjwa wa mwako wa tumbo na vidonda vya tumbo husababishwa na maambukizi ya bakteria tumboni.