STOCKHOLM : Mwanariwaya wa Uingereza ashinda tuzo ya Nobel ya fasihi
11 Oktoba 2007Mwandishi wa riwaya wa Uingereza Doris Lessing ameshinda Tuzo ya Nobel ya mwaka 2007 kwa fasihi.
Msemaji wa taasisi ya Royal Swedish Academy Horace Engdahl alitangaza uamuzi wa taasisi hiyo kwa tuzo hiyo yenye thamani ya dola milioni moja na laki tano.
Amesema Tuzo ya Nobel ya mwaka 2007 kwa fasihi atatunukiwa mwandishi riwaya wa Uingereza kwa Doris Lessing kwa kuufanya ulimwengu wa ustaarabu uliogawika uangaliwe kwa makini na nadharia ya kushuku,hamasa na nguvu ya njozi.
Lessing ambaye atatimiza umri wa miaka 88 hapo tarehe 22 Oktoba anakuwa mwanamke wa 11 kushinda tuzo hiyo tokea ilipozawadiwa kwa mara ya kwanza hapo mwaka 1901 na ushindi wake unakuja wiki hii ambapo wanasayansi wawili wa Ujerumani wametunukiwa tuzo za Nobel kwa fizikia na kemia.