1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Starmer atabiriwa kumbwaga Sunak uchaguzi Uingereza

4 Julai 2024

Waingereza wanapiga kura kwenye uchaguzi mkuu hivi leo, huku kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour akitabiriwa kumbwaga waziri mkuu wa sasa, Rishi Sunak, baada ya miaka 14 ya utawala wa chama cha Conservatives.

https://p.dw.com/p/4hqIt
Kiongozi wa upinzani wa Uingereza, Keir Starmer.
Kiongozi wa upinzani wa Uingereza, Keir Starmer.Picha: Cameron Smith/Getty Images

Uchunguzi wa maoni ya wapigakura unaonesha kwamba Keir Starmer atapata ushindi mkubwa kutokana na wapigakura kuchoshwa na wahafidhina, ambao wameonesha kiwango cha juu cha mgawanyiko uliosababisha Uingereza kuwa na mawaziri wakuu watano ndani ya kipindi cha miaka minane.

Soma zaidi: Labour yatabiriwa kuwagaragaza Conservative uchaguzi UK

Hata hivyo, uchunguzi huo wa maoni unaonesha kuwa wapigakura wanataka tu mabadiliko, na sio kwamba wanakiunga mkono chama cha Labour, kinachofuata siasa za mrengo wa kati kushoto.

Kwenye taarifa yake iliyotolewa leo, Starmer amewaambia wapigakura kwamba huenda leo, Uingereza ikaanza ukurasa mpya, lakini amewaonya kuwa hilo litawezekana tu endapo watajitokeza kwa wingi kupiga kura.