1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani aondolewa.

4 Oktoba 2023

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Marekani jana Jumanne wamemuondoa kwa kupiga kura spika Kevin McCarthy wa upande chama cha Republican mamlakani

https://p.dw.com/p/4X5Nx
USA | Repräsentantenhaus | Absetzung von McCarthy
Picha: Jonathan Ernst/REUTERS

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Marekani jana Jumanne wamemuondoa kwa kupiga kura spika Kevin McCarthy wa upande chama cha  Republican mamlakani katika kile kinachoelezwa kuwa zoezi la kihistoria kura.Kuondolewa kwa McCarthy kunaingia katika rekodi ya mwanzo kabisa katika historia ya Marekani ambapo spika, kiongozi wa wabunge wengi na wa pili kutoka kwa nafasi ya urais nyuma ya makamu wa rais kuondolewa madarakani.Baada ya zoezi la upigaji kura McCarthy aliwaambia waandishi wa habari kwamba anahitimisha muda wake wa kuwa spika wa bunge wa 55 ikiwa moja ya heshima kubwa aliyoipenda wakati wote.Kiini cha hatua hiyo ni Mbunge Matt Gaetz ambae Jioni ya Jumatatu alianzisha hoja ya kumuondoa spika huyo kutokana na kushirikiana na Wademokrat kupitisha mpango wa matumizi kwa siku 45 ili kuzuia kufungwa kwa shughuli za serikali.