Somalia: Hakuna nafasi ya upatanishi kati yetu na Ethiopia
18 Januari 2024Matangazo
Katika taarifa iliyochapishwa katika mitandao rasmi ya kijamii, wizara ya mambo ya nje ya Somalia imesema hakutokuwa na juhudi za upatanishi hadi pale Ethiopia itakapoyafuta makubaliano hayo na kuukubali tena kutambua uhuru wa kimipaka wa Somalia.
Mivutano katika eneo hilo la Pembe ya Afrika imeongezeka baada ya Ethiopia ambayo haina bahari kufikia makubaliano na Somaliland mnamo Januari mosi, makubaliano yaliyoipa ruhusa ya kuingia katika Bahari ya Shamu.
Rais wa Somalia afuta mkataba wa Somaliland na Ethiopia
Taarifa hii ya Somalia inakuja baada ya tawi la Umoja wa Afrika la usuluhishi wa mizozo kuujadili mzozo huo hapo jana na kutoa wito kwa nchi hizo mbili kufanya mazungumzo na kuchukua tahadhari ili kuzuia kutanuka kwa mzozo huo.