1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sita wafa kwa Marburg Rwanda

30 Septemba 2024

Waziri wa Afya wa Rwanda, Sabin Nsanzimana, amesema watu sita wamekufa kutokana na mripuko wa ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Marburg (MVD).

https://p.dw.com/p/4lEPv
Mchoro wa kirusi cha Marburg.
Mchoro wa kirusi cha Marburg.Picha: Science Photo Library/IMAGO

Akiandika kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa X, waziri huyo wa afya wa Rwanda amesema jumla ya watu 26 wamethibitishwa kuambukizwa ugonjwa huo.

Nsanzimana amesema wagonjwa 20 wanaotibiwa kwa sasa ni wafanyakazi wa afya na wametengwa huku uchunguzi wa kubaini chanzo cha mripuko huo ukiendelea.

Rwanda imeimarisha operesheni ya kuzuia kuenea ugonjwa huo katika vituo vyote vya afya.

Soma zaidi: Rwanda yathibitisha visa vya maambukizi ya virusi vya Marburg

Dalili za ugonjwa wa Marburg  ni pamoja na kuumwa na tumbo, kutapika na kuharisha damu, ambapo asilimia 88 ya walioambukizwa hufariki dunia, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Maambukizo kwa binadamu ni kwa njia ya kugusa maji maji ya mwili wa mtu aliyeambukizwa na inadhaniwa kwamba virusi hivyo vinasambazwa na popo.