1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Sita wafa kwa mafuriko Japan

23 Septemba 2024

Watu sita wamepoteza maisha kufuatia mvua kubwa, mafuriko na maporomoko ya udongo kwenye visiwa vya Japan.

https://p.dw.com/p/4kxRg
Mafuriko makubwa nchini Japan.
Mafuriko makubwa nchini Japan.Picha: ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Shirika la Habari la NHK limesema serikali ya kiisiwa cha mkoa wa Ishikawa imesema watu wawili hawajulikani walipo, na kuifanya idadi ya wasiofahamika hatima zao kufikia watu wanane.

Mkoa huo ambao bado ulikuwa unaendelea kujengwa tena baada ya tetemeko la ardhi la mapema mwaka huu lililosababisha tsunami na moto mkubwa, umeendelea kushuhudia mvua ya masaa 72 mfululizo.

Soma zaidi: Watoto milioni sita waathiriwa na Kimbunga Yagi

Mafuriko yamezifunika nyumba za dharura zilizokuwa zikiwahifadhi wale walioathirika na tetemeko hilo la ardhi lililouwa watu 374 kwenye Mkesha wa Mwaka Mpya.

Zaidi ya nyumba 4,000 kwenye mji mkuu wa mkoa huo, Wajima, hazina huduma ya umeme kutokana na mafuriko hayo.