1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SIPRI: Idadi ya silaha za nyuklia kuongezeka duniani

13 Juni 2022

Katika ripoti mpya ya kila mwaka Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Sweden- SIPRI imekadiria kuongezeka tena kwa idadi ya silaha za nyuklia kwa hivi karibuni kutokana na ulimwengu kugubikwa na mivutano.

https://p.dw.com/p/4CbVk
BG Nuklearwaffen | indische Agni-V Rakete
Picha: Manish Swarup/AP/picture alliance

Pamoja na kupungua kwa kiwango kidogo sana cha jumla ya idadi ya vichwa vya nyuklia kwa  wastani wa vichwa 12,705 duniani kote, lakini watafiti wa SIPRI katika ripoti yao ya leo hii wanadhani idadi hiyo itaongezeka tena katika kipindi cha muongo ujao.

Mtaalamu wa taasisi hiyo, Hans Kristensen amesema kumekuwa na dalili za wazi kwamba hali ya kupungua kwa silaha za nyuklia, tangu kumalizika kwa Vita Baridi imefikia ukomo. Na mwenza wa mtaalamu huyo kikazi, Matt Korda aliongeza kusema endapo mataifa yenye silaha za nyuklia hayatachukua hatua za haraka katika umadhubuti wa kudhibiti ongezeko la silaha hizo basi idadi ya yichwa vya nyuklia inaweza kuongezeka kwa mara ya kwanza tangu kumalizika zama za Vita Baridi.

Urusi na Marekani bado zina idadi kubwa ya vichwa vya nyuklia.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya mwaka wa SIPRI iliyowekwa hadharani leo hii, Urusi ina vichwa 5,977 na Marekani 5,428 ambavyo vikijumuishwa pamoja mataifa hayo yanamiliki asilimia 98 ya karibu vichwa vyote vya nyuklia duniani. Kwa mwaka 2021 idadi ya vichwa vya nyuklia kwa mataifa yote hayo ilipungua zaidi na hilo lilitokana na hatua ya kuviteketeza, na hasa vile ambavyo vilitelekezwa kwa matumizi ya kijeshi kwa miaka mingi.

Atomrakete Pakistan Flash-Galerie
Jaribio la kombora nchini PakistanPicha: AP

Lakini hata hivyo hazina ya silaha iliyopo ambayo inaweza kutumika kijeshi kwa mataifa hayo imeendelea kusalia kuwa madhubuti. Kwa mujibu wa SIPRI mataifa hayo kadhalika yanaendeleza programu kubwa na za ghamara zinazoendeleza kubadilisha na kuboresha vichwa vya nyuklia pamoja na vifaa vya uzalishaji.

Mataifa mengine saba yanaendelea na mipango ya nyuklia.

Rekodi zinanesha matiafa mengine 7 yenye silaha za nyuklia ni Uingereza, Ufaransa, China, India, Pakistan, Israel na Korea Kaskazini. Yote kwa pamoja yanaripotiwa kuwa uendelezaji au mifumo mipya ya silaha. Mtafiti wa taasisi SIPRI, Kristensen anasema hakuna taifa lolote miongoni mwa hayo lenye nia ya kuachana na silaha za nyuklia kwa namna yoyote ile.

Kinyume chake, China ipo katikati ya mpango wa upanuzi wa kina wa silaha zake,mwaka 2021 Uingereza imetangaza itapanua ukomo wa uhifadhi wake wa vichwa vya nyuklia.

Soma zaidi:Matumizi ya kijeshi yaongezeka duniani-SIPRI

Kwa miongo kadhaa, idadi ya silaha za nyuklia duniani kote imekuwa kupungua kwa kasi. Hesabu zake kwa kiwango hicho kinaweza kuwa chini ya moja ya tano ya kile kilichokuwa katika kilele cha Vita Baridi kwenye 1980.

Chanzo DPA.