Jumatano ni siku ya kimataifa ya kupinga unyanyasaji kwa ya waandishi habari unaokwenda bila kuadhibiwa. Sambamba na siku hii, shirika la UN la Elimu na Sayansi, UNESCO limesema 86% ya mauaji dhidi ya waandishi wa habari duniani hupita bila kushughulikiwa. Je hali ikoje katika ukanda wa Afrika? Msikilize Salome Kitomari mwenyekiti wa taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika na Daniel Gakuba.