Siku 6 za kuweka chini silaha zaelekea ukingoni Syria
29 Oktoba 2019Makubaliano ya kusitisha mapigano yalipaswa kuanza kutekelezwa Oktoba 22 takribani majuma mawili baada ya serikali ya Uturuki kuanzisha mashambulizi makali ya kijeshi dhidi ya kundi hilo,yaliyokosolewa na mataifa kadhaa ulimwenguni. Kwa mujibu wa makubaliaono haya wapiganaji wa kundi la YPG lilipaswa kuwa na muda hadi wa saa 12 jioni ya leo kuondoka katika Kaskazini Mashariki mwa Syria.
Wapigaji wa YPG walipambana na IS
Kundi la wanamgambo wa YPG,ndio lilikuwa jeshi lenye kutegemewa katika vita ya ardhini katika kukabiliana na Kundi la Dola la Kiislamu nchini Syria, ambalo lilikuwa linaungwa mkono na mataifa ya magharibi na vikosi maalumu. Lakini serikali ya Uturuki inaliunganisha kundi hilo na lile la Uturuki la chama PKK, ambalo wao, Uturuki, Umoja wa Ulaya na hata Marekani.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amerudia mara kadhaa kutoa kutishia kuanzisha tena mashambulizi dhidi ya wanamgambo hao ikiwa hawajaondoka kwenye eneo hilo kufikia muda wa mwisho uliowekwa.Jana waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu alisistiza onyo lililotolewa na rais Erdogan. Urusi imelipa onyo kundi hilo kwamba majeshi yake na ya Syria yameweka kambi kwa muda katika eneo hilo ili kuweza kuhakiki, hatua ya uondokaji na salama kwa kutoa ulinzi.
Hatua za kuondoma zimeanza kuonekana
Sergey Romanenko anaongoza kitengo cha maridhiano cha Urusi. alisema "Wakurud wa kikosi cha YPG na mifumo yao ya silaha, wanapaswa kuondoka katika maeneo ya Tell Rifat na Manbiji. Tunaamini, kuondoka kwao kutachangia kuleta hali ya utulivu katika eneo la mpaka wa Uturuki na Syria" alisema askari huyo. Mapema hapo jana Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Minister Mevlut Cavusoglu alirejea upya onyo la Erdogan kwamba endapo masaa 150 yatamalizika, na kundi la YPG alijasalimu amri katika eneo la mpakani. Uturuki itasafisha safisha, magaidi wote katika eneo hilo.
Katika hatua nyingine maafisa wa Marekani wamesema mwili wa aliyekuwa kiongozi wa kundi la Dola la Kiislamu Abu Bakr al-Baghdadi. umezikwa katika eneo la bahari ikiwa ni habari mpya, kabisa ikikihusu kikosi maalumu cha Marekani, ambacho kiliongoza uperesheni iliyopelekea kifo chake. Jamii ya Wakurd, kutoka upande wa Syria ndio yenye kudaiwa kuwa chanzo muhimu cha ujasusi, ambacho kiliiongoza Marekani katika jitihada za kumsaka Baghdadi ambae amekuwa akiongoza matukio ya kigaidi katika maeneo ya Iraq na Syria.