Sigmar Gabriel ajitoa kushiriki serikali mpya
8 Machi 2018Siku ya Alhamis Gabriel alitumia mtandao wa kijamii wa Twitter kutuma ujumbe wake kwa umma kwamba hatokuwa mmoja wa wajumbe wa SPD katika serikali mpya ya Ujerumani.
Ametaka chama chake, mbali ya kuwa aliwahi kuwa mwenyekiti wa chama hicho cha SPD, kukifahamisha wazi. Kwasababu uongozi mpya wa Olaf Scholz na mwenyekiti mtarajiwa Andrea Nahles unataka hadi ifikapo kesho Ijumaa asubuhi kutangaza, nani watakuwamo katika baraza la mawaziri la kansela Angela Merkel. Na nani anaondoka. Lakini kuhusiana na mipango ya Sigmar Gabriel,ameamua hatahusika. Na amekwisha amua.
Kwa hivi sasa Gabriel ndie mwanasiasa anayependwa sana. Amefanikisha kuachiwa huru kwa mwandishi habari raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki Deniz Yücel kupitia diplomasia makini. Kutokana na hatua za uwazi alizozichukua kufanikisha jambo hilo hakuna mtu atakayemsahau. Hakutafuna maneno inapokuja suala la Donald Trump.
Anafanya ziara huku na huko bila kuchoka, kwenda Moscow, na hadi katika mataifa ya eneo la Balkan. Na kwa muda mfupi kabisa ameweza kupambana na wanachama muhimu wa chama hicho. Kwanza alimfanya Martin Schulz kuwa mwenyekiti wa chama na mgombea wa kiti cha ukansela, na kuchafua kampeni za uchaguzi. Kwanini ? kama kuna mtu anayefahamu.
Bado gharama zaidi zinawezekana ? Mara Gabriel huwa mtetezi wa sera za kiliberali za wakimbizi za kansela na kubandika kabisa kauli mbiu ya wakimbizi mnakaribishwa wakati wa kikao cha bunge la Ujerumani Bundestag, na kisha anaonya dhidi ya kuwakandamiza Wajerumani kuhusiana na kipato chao kidogo kwa kuruhusu wahamiaji wengi.
Baada ya kushindwa uchaguzi
Amesafiri kwenda Cairo na kukosoa wakati akiwa bado katika ndege kukamatwa watu wengi na utawala wa Abdel Fattah el-Sisi, na kisha kusema mbele ya waandishi habari kwamba amefurahishwa na rais huyo. Unaweza kuzunguka katika, duara bila kuonesha mwelekeo halisi, na kuacha mawazo yako yakielea.
Baada ya kushindwa vibaya chama chake katika uchaguzi wa mwezi Septemba mwaka jana alikishambulia chama chake cha Social Democratic , kwa kuchagua watu ambao sio sahihi, na kukumbatia misimamo ambayo si sahihi. Kwa neno moja: Kuwashawishi zaidi wale wote ambao hawaridhishwi kama vile kuwawekea mazingira mazuri ya watu kupata mishahara bora ama matibabu mazuri nchini.
Na tusisahau kwamba , alikuwa mkuu wa chama hicho kwa muda wa miaka minane, muda mrefu zaidi kuliko mwenyekiti yeyote mwingine wa chama hicho baada ya Willy Brandt.
Ni mtu ambaye anaweza kuwa wa utata, kwa mambo yake. Anachanganya mambo ya kisiasa na ya binafsi, anamuingiza mtoto wake wa kike katika masuala ya umma, wakati alipomwambia , anapaswa sasa kutumia muda wake mwingi zaidi kwa mwanae na asimwache pamoja na yule mtu mwenye madevu. Alikuwa na maana ya Martin Schulz.
Maneno ya kejeli kabisa. Gabriel anaomba radhi , kila mara. Anabahati mbaya , kama ilivyo hivi sasa kwamba Andrea nahles ndie mkuu wa chama hicho, ambaye alikuwa katibu mkuu wa chama chini ya uongozi wa Gabriel kipindi ambacho alifanyakazi kwa nguvu zote. Mara nyingi alifanya aonekane kama mwanafunzi msichana. Kwa kuwa gabriel hakuweza kumvumilia karibu akiwa karibu yake, na hakuwahi kumuona kama kiongozi anayelingana nae.
Mwandishi: Thurau, Jens / ZR/ Sekione Kitojo
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman