JangaBrazil
Shughuli zasimama Brazil huku mvua ikiendelea kunyesha
14 Mei 2024Matangazo
Zaidi ya watu milioni mbili wameathirika na mafuriko katika jimbo la Rio Grande do Sul, ambapo miji na sehemu ya mji mkuu wa jimbo hilo imefurika maji kwa takriban wiki mbili sasa.
Zaidi ya watu 600,000 wamepoteza makao kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo huku timu ya waokoaji wakitafuta watu 127 walioripotiwa kupotea.
Soma pia: Rais Lula alirai bunge kutangaza janga baada ya mafuriko
Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amekiri kuwa mamlaka nchini humo haikuwa imejitayarisha kwa janga kubwa kama hilo.
Mvua hiyo iliyosababisha mafuriko ni dhoruba ya hivi karibuni kuikumba Brazil baada ya nchi hiyo kukumbwa pia na moto wa misitu na wimbi la joto huku wataalamu wakifungamanisha matukio hayo na athari ya mabadiliko ya tabia nchi.