1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSomalia

UNICEF yasikitishwa na adhabu ya kunyongwa nchini Somalia

23 Agosti 2024

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeelezea masikitiko makubwa juu ya kunyongwa kwa vijana wanne nchini Somalia wanaohusishwa na kundi la wanamgambo la Al-Shabaab.

https://p.dw.com/p/4jpH7
Wanamgambo wa Somalia
Wanamgambo wa al-Shabaab kama wanavyoonekana pichani, Februari 17, 2011 wakifanya mazoezi katika viunga vya MogadishuPicha: picture alliance / AP Photo

Vijana hao waliuawa kutokana na makosa wanayodaiwa kuyatenda wakati walipokuwa chini ya umri wa miaka 18.

Katika taarifa yake, UNICEF imesema hukumu ilitolewa na mahakama za kijeshi, ambazo hazina taratibu maalum zinazojali haki ya mtoto.

Aidha, UNICEF imezitolea wito mamlaka za jimbo la Puntland kuwachukulia watoto wanaohusishwa na makundi yenye silaha kama wahanga.

Jumla ya wapiganaji 10 wa Al-Shabaab waliuawa kwa kupigwa risasi siku ya Jumamosi baada ya kuhukumiwa kifo na mahakama ya kijeshi ya Puntland kwa mauaji na milipuko ya mabomu katika mji wa Galkayo.