1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Shirika la Ujerumani lasema hali inazidi kuwa mbaya Sudan

Hawa Bihoga
17 Februari 2024

Mkuu wa shirika lisilo la kiserikali nchini Ujerumani la Welthungerhilfe amesema hali nchini Sudan inazidi kuwa mbaya katikati wakati vita havioneshi dalili ya kumalizika.

https://p.dw.com/p/4cWpY
Maakazi ya muda ya wakimbizi wa mzozo wa Sudan
Hali ya maisha ya watoto na raia waliopoteza makaazi kutokana na vita nchini SudanPicha: Marwan Ali/AP/picture alliance

Katibu Mkuu wa shirika hilo Matthias Mogge, ambae amerejea kutoka ziarani nchini humo ameelezea hali ya kufurika kwa kambi za wakimbizi, ugumu wa kusambaza misaada ya kiutu na kuendelea kwa mapigano makali ya wenyewe kwa wenyewe.

Mogge ameongeza kuwa wafanyakazi wa mashirika ya misaada ya kiutu wanakabiliwa na changamoto kubwa na hali katika jimbo la magharibi la  Darfur ni janga kutokana na kuongezeka kwa njaa.

Sudan imekumbwa na mzozo kufuatia mapigano kati ya Kiongozi mkuu wa Sudan, Abdel Fattah al-Burhan na makamu wake wa zamani ambae pia ni kiongozi wa wanamgambo wa RSF kupigania madaraka tangu mwezi April 2023.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa takriban watu milioni 8 wamekuwa wakimbizi kufuatia mapigano hayo.