MigogoroSyria
Waasi nchini Syria wadhibiti eneo kubwa la Aleppo
30 Novemba 2024Matangazo
Shirika la Uangalizi wa Haki za Binadamu nchini Syria limesema makundi ya Hayat Tahrir al-Sham (HTS) na washirika wao yameteka sehemu kubwa za mji huo pamoja na vituo vya serikali na magereza.
Waasi hao wameendelea kushambulia vikosi vya serikali vinavyosaidiwa na Iran na Urusi tangu Jumatano, siku ambayo usitishaji vita ulianza rasmi nchini Lebanon kati ya Israel na Hezbollah inayoungwa mkono na Iran.
Urusi ilifanya mashambulizi ya angani usiku kwenye maeneo ya Aleppo kwa mara ya kwanza tangu 2016, na kufikisha idadi ya vifo 311, vikiwemo vya wanajeshi 100, raia 28, na wanamgambo wa HTS na washirika wao 183.