1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shirika la FAO lasema bei ya chakula ilishuka Desemba

3 Januari 2025

Faharasa ya bei ya chakula duniani ya Umoja wa Mataifa ilishuka mwezi Desemba ikilinganishwa na viwango vya Novemba, kutokana na kushuka kwa bei ya sukari kimataifa.

https://p.dw.com/p/4omoY
Bei ya chakula duniani ilishuka mwezi Desemba ikilinganishwa na viwango vya Novemba
Bei ya chakula duniani ilishuka mwezi Desemba ikilinganishwa na viwango vya NovembaPicha: Benefit-Sharing Fund BSF/FAO

Hayo ni kulingana na takwimu zilizotolewa leo na Shirika la Chakula Duniania, FAO.

Faharasa ya FAO inayofuatilia bidhaa za chakula zinazouzwa duniani, ilipungua hadi alama 127.0 mwezi Desemba, kutoka 127.6 mwezi Novemba.

Kwa mwaka wote wa 2024, faharasa ilikuwa wastani wa alama 122.0, ikiwa ni asilimia 2.1 chini ya mwaka 2023, kutokana na kupungua kwa bei ya nafaka na sukari, na kuongezeka kidogo bei za mafuta yatokanayo na mboga maziwa na nyama.

Bei ya sukari ilisababisha kushuka viwango vya Desemba kwa asilimia 5.1 kutokana na kuongezeka kwa kilimo cha zao la miwa katika nchi zinazolima kwa wingi zao hilo hadi kufikia asilimia 10.6, chini ya kiwango cha Desemba mwaka 2023.