1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBangladesh

Sheikh Hasina ashinda uchaguzi wa Bunge nchini Bangladesh

8 Januari 2024

Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina, ameshinda kwa kishindo uchaguzi wa Bunge uliogubikwa na vurugu na kususiwa na chama kikuu cha upinzani.

https://p.dw.com/p/4axW7
Bangladeschs Premierministerin Sheikh Hasina zeigt ihren Stimmzettel
Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina akipiga kura mjini Dhaka: 07.01.2024Picha: Altaf Qadri/AP

Ushindi huu unampa yeye na chama chake cha "Awami League" muhula wa tano mfululizo madarakani.

Wakati matokeo ya mwisho na takwimu kamili zikitarajiwa kutangazwa rasmi katika sherehe baadaye leo, maafisa wa tume ya uchaguzi wamesema  chama cha Hasina kimeshinda karibu robo tatu ya viti bungeni, ikiwa ni sawa na angalau viti 220 kati ya 300.

Chama cha Hasina hakikukabiliwa na upinzani mkubwa katika viti kinavyopigania lakini kimejiepusha kuweka wagombea katika baadhi ya majimbo ili kuepusha bunge kuonekana kuwa linadhibitiwa na chama kimoja.

Hasina amesimamia ukuaji uchumi katika taifa ambalo liliwahi kukabiliwa na umaskini uliokithiri lakini serikali yake imetuhumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu na ukandamizaji mkali dhidi ya upinzani.