1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shehena ya kwanza ya chanjo za Mpox kuwasili leo Kongo

Sylvia Mwehozi
5 Septemba 2024

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leo itapokea shehena ya kwanza ya dozi takribani 100,000 za chanjo ya Ugonjwa wa homa ya nyani Mpox.Seŕikali ya Kongo imepanga kuanza zoezi la utoaji wa chanjo ya Mpox mwishoni mwa juma.

https://p.dw.com/p/4kHws
Kongo -Mpox
Mgonjwa wa Mpox-KongoPicha: WHO/Aton Chile/IMAGO

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leo itapokea shehena ya kwanza ya dozi takribani 100,000 za chanjo ya Ugonjwa wa homa ya nyani Mpox. Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Afrika CDC, kimeongeza kuwa jumla ya chanjo laki 200,000 zitawasili nchini humo kufikia mwishoni mwa wiki hii.

Soma: WHO : Afrika inaweza kutokomeza Mpox ndani ya miezi sita

Shehena ya kwanza iliyobeba chanjo za Mpox itawasili mjini Kinshasa majira ya saa tano asubuhi, huku ndege nyingine iliyobeba chanjo laki 200,000 imepangwa kuwasili kabla ya mwisho wa wiki hii. Seŕikali ya Kongo imepanga kuanza zoezi la utoaji wa chanjo ya Mpox mwishoni mwa juma. Chanjo hizo za kwanza zinatoka katika kampuni ya dawa ya Bavarian Nordic ya Denmark. Zaidi ya visa 17,500 na vifo 629 vimeripotiwa nchini humo tangu mwaka huu uanze kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO.