1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Sharif ataka bunge Pakistan kumchukulia hatua Khan

28 Machi 2023

Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif ameliomba bunge kumchukulia hatua mtangulizi wake, Imran Khan, akidai chama chake kimehusika katika vurugu zilizozuka wakati polisi walipojaribu kumkamata kwa tuhuma za ufisadi.

https://p.dw.com/p/4POAe
Pakistan Shehbaz Sharif
Picha: Fabrice Coffrini/AFP

Vurugu hizo zilizuka mwanzoni mwa mwezi huu wakati wafuasi wa Imran Khan walipojaribu kuwazuia polisi kumkamata kiongozi huyo wa zamani.

Siku ya Jumanne (Machi 28), Sharif aliliomba bunge limchukulie hatua Khan lakini hakutaja ni hatua gani zichukuliwe. 

Baadhi ya mawaziri katika serikali yake wametowa mwito wa kuchukuliwa hatua ya kupigwa marufuku chama cha Khan cha Tehreek-e-Insaf (PTI) kinachodaiwa kuwa na wanamgambo miongoni mwa wanachama wake.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW