1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Shambulizi la droni la Urusi lawajeruhi watu tisa mjini Kyiv

Josephat Charo
30 Oktoba 2024

Shambulizi la Urusi mjini Kyiv usiku wa kuamkia leo limewajeruhi watu tisa, akiwemo msichana wa umri wa miaka 11.

https://p.dw.com/p/4mOUX
Ukraine | shambulio la droni Kyiv
Mashambulizi ya Urusi yamelenga mindombinu ya kiraia na nishati.Picha: State Emergency Service of Ukraine/Handout/REUTERS

Taarifa hiyo imetolewa na maafisa wa Ukraine wakati Urusi ikiongeza mashambulizi yake ya kutokea angani dhidi ya mji mkuu huo wa Ukraine.

Maafisa wa mamlaka ya jiji na wa huduma za dharura wamesema moto mkubwa ulizuka ndani ya jengo la ghorofa tisa katika wilaya ya katikati na shule ya chekechea ilikuwa imeharibiwa.

Soma pia: Putin aonya juu ya Ukraine kutumia makombora ya masafa marefu

Meya wa mji wa Kyiv Vitali Klitschko amesema mabaki ya droni iliyokuwa imeharibiwa yalisababisha uharibifu huo. Jeshi la anga la Ukraine limesema limezitungua droni 33 kati ya 62 zilizorushwa na vikosi vya Urusi katika maeneo kumi na katika mji mkuu Kyiv.

Wizara ya ulinzi ya Urusi kwa upande wake imesema imefanikiwa kuziangusha droni 23 za Ukraine usiku wa kuamkia leo zilizokuwa zimevurumishwa katika himaya ya Urusi.