1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Shambulio la Urusi laua na kujeruhi watu huko Kyiv, Ukraine

18 Januari 2025

Watu watatu wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa katika shambulio la kombora la Urusi kwenye mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesema hayo kwenye mtandao wa kijamii wa X.

https://p.dw.com/p/4pK5x
Kyiv I Ukraine
Uharibifu wa moja ya jengo mjini Kyiv kufuatia shambulio la UrusiPicha: Efrem Lukatsky/AP/picture alliance

Watu watatu wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa katika shambulio la kombora la Urusi kwenye mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, Rais
Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesema hayo hii leo katika chapisho lake kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Mamlaka ya kijeshi imesema kituo cha metro cha Lukianivska kilichopo karibu na jiji la Kyiv kimefungwa kutokana na uharibifu mkubwa wa mashambulizi hayo ya Urusi. Kituo hicho kipo karibu na kiwanda cha kutengeneza silaha ambacho kimekuwa kikilengwa mara  kadhaa na mashambulio ya makombora ya Urusi.

Soma zaidi. Urusi yaushambulia mji mkuu wa Ukraine, watu watatu wauawa

Wizara ya ulinzi ya Urusi yenyewe imesema kwamba shambulio lake hilo kwenye kiwanda hicho cha kutengeneza silaha za masafa marefu aina ya Neptune kimeharibiwa kwa kiwango kikubwa.

Kwingineko, Rais Zelensky amesema watu 10 wamejeruhiwa katika shambulio la Urusi katika mji wa kusini mwa Ukraine wa Zaporizhia, pamoja na uwezekano wa wengine kuwa bado chini ya kifusi.