1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Israel yaidhinisha mpango wa kutanua makazi eneo la Golan

15 Desemba 2024

Serikali ya Israel imeidhinisha hii leo mpango wa kutanua makazi ya Israeli kwenye Milima ya Golan, ikisema imechukua hatua hiyo "kwa kuzingatia vita na kitisho kipya kinachoibuliwa na Syria".

https://p.dw.com/p/4oATm
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kujiimarisha katika eneo la Golan ni kuimarisha Taifa la IsraelPicha: Uncredited/Israeli Government Press Office/AP/dpa/picture alliance

Aidha imesema hatua hiyo inalenga kutimiza azma yake ya kuongeza idadi ya watu wake mara mbili kwenye eneo la Golan.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kujiimarisha kwenye eneo la Golan, ni sawa na kuliimarisha Taifa la Israel, na ni hatua muhimu hasa katika kipindi hiki.

Amesisitiza kwamba wataendelea kulishikilia eneo hilo, kuimarika zaidi na kulifanya kuwa makazi yao.