Serikali ya Burundi kususia mazungumzo ya amani
16 Februari 2017Matangazo
Mazungumzo hayo yanalenga kutafuta suluhu katika mzozo wa kisiasa uliosababisha umwagikaji wa damu ambao ulianza mwaka 2015 baada ya Rais Pierre Nkurunziza kusema atawania muhula wa tatu madarakani, hatua ambayo wapinzani wamesema inakiuka katiba na makubaliano ya amani yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo. Serikali imekuwa ikiushutumu Umoja wa Mataifa kwa kufanya upendeleo dhidi yake baada ya makundi kadhaa ya haki za binadamu kusema majeshi ya usalama na chama tawala yamejihusisha na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu. Msemaji wa serikali Phillipe Nzobonariba amesema serikali inapinga kuwapo kwa mshauri mwandamizi wa Umoja wa Mataifa Benomar Jamal katika mazungumzo hayo yanayofanyika mjini Arusha,Tanzania.