1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Seoul:Huenda wanajeshi wa Korea Kaskazini wanapigana Ukraine

8 Oktoba 2024

Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imesema kuna uwezekano mkubwa kuwa wanajeshi wa Korea Kaskazini wanapigana nchini Ukraine kuisaidia Urusi na kwamba baadhi yao tayari wameuawa.

https://p.dw.com/p/4lX0q
Wanajeshi wa Korea Kaskazini
Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Korea (KPA) wakijiandaa kufyatua silaha zao wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 64 tangu kuanza kwa Vita vya Korea, Juni 25, 2014.Picha: Jon Chol Jin/AP Photo/picture alliance

Vyombo vya habari vya Ukraine vimeripoti kuwa mnamo Oktoba 3, maafisa sita wa kijeshi wa Korea Kaskazini waliuawa katika shambulio la kombora karibu na mkoa wa Donetsk. Hapo jana, Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alimtumia ujumbe wa kheri wa siku ya kuzaliwa Rais wa Urusi Vladimir Putin akimuita mshirika wake wa karibu huku akisema pia kuwa nchi yake itachukua hatua za haraka kuelekea kuimarisha jeshi lake na silaha za nyuklia.