1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Seneti ya Marekani kumuhoji naibu mkurugenzi wa CIA

Josephat Charo
30 Julai 2024

Wabunge wa baraza la seneti wanatarajiwa kumhoji kaimu mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Marekani CIA Ronald Rowe kuhusu mapungufu ya utekelezaji wa sheria saa chache kuelekea jaribio la kutaka kumuua Donald Trump.

https://p.dw.com/p/4ivIp
Marekani |Kongamano la Chama cha Republican huko Milwaukee | Donald Trump
Mgombea urais wa chama cha Republican Rais wa zamani Donald Trump, akihudhuria siku ya kwanza ya Kongamano la Kitaifa la Republican, Jumatatu, Julai 15, 2024.Picha: Carolyn Kaster/AP Photo/picture alliance

Hii ni hatua ya hivi karibuni ya mfululizo wa vikao vya uchunguzi wa shambulizi hilo la risasi lililotokea Julai 13. Rowe alichukua nafasi ya kaimu mkurugenzi wa CIA wiki iliyopita baada ya mtangulizi wake Kimberly Cheatle kujiuzulu kufuatia kikao cha bunge ambapo alihojiwa na wabunge wa vyama vya Democratic na Republican na akashindwa kujibu masuala maalumu kuhusu mapungufu ya mawasiliano kabla shambulizi hilo. Rowe anataamandamana na Naibu Mkurugenzi wa shirika la upelelezi wa ndani FBI Paul Abbate katika kikao cha pamoja cha kamati za baraza la seneti zinazoshughulikia wiazara ya sheria na wizara ya usalama wa ndani.