1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Senegal yaanza vyema AFCON, Cameroon, Algeria zakwaa kisiki

16 Januari 2024

Timu ya soka ya Senegal imeanza vyema michuano ya mataifa ya kombe la Afrika, AFCON, kwa kuicharaza Gambia mabao 3-0 katika mchezo wa jana jioni uliopigwa kwenye mji mkuu wa Ivory Coast, Yamoussoukro.

https://p.dw.com/p/4bHmf
Kandanda | AFCON | Senegal vs Gambia
Wachezaji wa Senegal wakifurahia moja ya mabao waliyofunga kwenye mchezo na Gambia katika michuano ya AFCON huko Ivory Coast.Picha: Issouf Sanogo/AFP/Getty Images

Senegal ambayo ni mabingwa watetezi wa kombe la AFCON wanatumai kulitwaa tena taji hilo kwenye mashindano ya mwaka huu. Kwenye mchezo wa jana ilikuwa dhahiri kuwa timu hiyo ya mshambuliaji Sadio Mane iliwadhibiti vilivyo wenzao wa Gambia, timu iliyopitia vizingiti vingi kuelekea michuano ya AFCON.

Ushindi huo wa Simba wa Teranga unawaweka mbele kwenye kundi C hasa baada ya timu nyingine za kundi hilo Cameroon na Guinea kutunishiana misuli na kutoka sare ya bao 1-1.

Kulikuwa na mchezo mwingine jana usiku kati ya Algeria na Angola kutoka kundi D ambao pia ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.