1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz: Kauli ya Trump kuhusu NATO ni ya kutowajibika

13 Februari 2024

Kansela wa wa Ujerumani, Olaf Scholz jana Jumatatu amelaani tishio la mtarajiwa wa urais wa Marekani Donald Trump la kutowalinda wanachama wa NATO ambao hawachangii fedha za kutosha katika ulinzi wa jumuiya hiyo.

https://p.dw.com/p/4cKm8
USA Washington 2024 | Uwanja wa ndege wa kuwasili | Kansela Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz (SPD) wakati akiwa katika ziara yake mjini Washington Marekani. Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Akizungumza baada ya mkutano wake na Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk amesema uhusiano wa pamoja usio wa uwajibikaji kwa NATO ni hatari na utakuwa na manufaa tu, kwa upande wa Urusi.Jumamosi iliyopita Trump alitoa kitisho cha kwamba  iwapo atachaguliwa tena nchini Marekani, hatawatetea wanachama wa NATO ambao hawajatimiza wajibu wao wa kifedha, na kwenda mbali zaidi kwa kauli iliyoonesha kama akihimiza Urusi kuwashambulia.