1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz asema mazungumzo magumu juu ya bajeti yanaendelea

26 Juni 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema mazungumzo ndani ya vyama vitatu vinavyounda serikali ya mseto kuhusu bajeti ya serikali ya mwaka 2025 yanaendelea licha ya kuwepo ripoti za mkwamo.

https://p.dw.com/p/4hXgj
Berlin | Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz Picha: Political-Moments/IMGAO

Scholz, katika hotuba aliyoitoa bungeni, amesema kunafanyika mazungumzo ya siri na yenye kuzingatia uhalisia wa mambo juu ya bajeti ya mwaka ujao na kifurushi kinachokusudiwa kupiga jeki uchumi wa taifa hilo. 

Kiongozi huyo wa Ujerumani ameeleza kuwa watawasilisha rasimu ya bajeti hiyo mwezi ujao.

Ujerumani yatupilia mbali miito ya kuitisha uchaguzi wa mapema

Scholz, Makamu wa Kansela Robert Habeck wa chama cha kijani na Waziri wa fedha Christian Lindner kutoka chama cha Waliberali, FDP, walikuwa wamepanga kuwasilisha bajeti katika mkutano wao wa Julai 3.

Hata hivyo, kukosekana kwa muafaka juu ya bajeti hiyo, kunamaanisha kuwa sasa baraza la mawaziri litawasilisha bajeti hiyo mnamo Julai 17.