1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz arejelea wito wa mkutano wa amani kuhusu Ukraine

11 Septemba 2024

Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani leo kwa mara nyingine amerejelea mwito wake wa kuandaa mkutano mwingine wa amani wa kumaliza vita vya Urusi vinavyoendelea nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4kV29
Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani
Kansela Olaf Scholz wa UjerumaniPicha: Ebrahim Noroozi/AP Photo/picture alliance

Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani leo kwa mara nyingine amerejelea mwito wake wa kuandaa mkutano mwingine wa amaniwa kumaliza vita vya Urusi vinavyoendelea nchini Ukraine, utakaoikaribisha mezani Urusi.

Akizungumza bungeni, mjini Berlin kiongozi huyo wa Ujerumani amesema huu ndio wakati wa kutumia fursa zilizobakia. Scholz amekiri kwamba baadhi ya wapiga kura hawaungi mkono hatua ya kuipatia msaada wa kijeshi Ukraine na wamekuwa wakiunga mkono vyama vinavyoendesha kampeni dhidi ya hatua hiyo. Hata hivyo, amesisitiza kwamba kuchukuwa hatua ya kuisadia Ukraine ndio jambo sahihi pale inapohitajika.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW