Scholz alihutubia bunge kuhusu mgogoro wa bajeti
28 Novemba 2023Kiongozi huyo amelihutubia mapema leo bunge la Ujerumani kuhusu mgogoro wa bajeti ya serikali yake ya mseto.
Mjadala wa saa mbili bungeni umepangwa kufuatia taarifa ya Kansela huyo. Inatarajiwa kuwa, kambi ya upinzani itaishambulia serikali kwa kujaribu kutafuta njia za kusimamisha utekelezaji wa ibara ya katiba inayoweka ukomo wa deni la taifa.
Soma pia:Serikali ya Ujerumani yaidhinisha bajeti ya ziada na kuepusha mgogoro
Mahakama ya kikatiba ya shirikisho ilitoa uamuzi kwamba serikali ya Kansela Olaf Scholz ilivunja masharti ya katiba kupitia azma yake ya kuhamisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya kukabiliana na janga la Corona kwenda kwenye mfuko wa kupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Uamuzi huo wa mahakama uliiacha serikali kuu na pengo la euro bilioni 60 katika bajeti yake na hivyo basi kutilia shaka uwezekano wa kuendelea na miradi ya maendeleo na uwekezaji.