Scholz akwepa kumtaja wanaemuunga mkono Umoja wa Ulaya
11 Juni 2024Hayo yametokea siku moja tu, baada ya uchaguzi wa bunge la Umoja wa Ulaya. Scholz alirudia msimamo wake wa awali kwamba urais wa kamisheni lazima uwe na uungawaji mkono wa msingi wa wingi wa kidemokrasia wa kijadi katika Bunge la Ulaya. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Berlin akiwa na Rais wa Chile anayezuru nchini Ujerumani, Gabriel Boric, Scholz amesema, hata hivyo upo uwezekano wa kuzingatia kumuunga mkono sambamba nawagombea mbalimbali wa nafasi za juu za Umoja wa Ulaya katika majuma yajayo.Von der Leyen, mwanasiasa wa Ujerumani na waziri wa zamani kutoka chama cha kihafidhina cha Conservative Christian Democrats (CDU), alitoa wito kwa vyama vya kidemokrasia na vya kiliberali vya Umoja wa Ulaya kuunga mkono azma yake ya kuwania tena kiti cha halmashauri kuu ya umoja huo.