Scholz aanza kusaka waziri mpya wa ulinzi
16 Januari 2023Naibu msemaji wa Kansela Scholz, Christiane Hoffmann amesema kiongozi huyo wa Ujerumani anaheshimu maamuzi ya Lambrecht na amemshukuru kwa kazi nzuri aliyoifanya akiwa waziri wa ulinzi.
''Kama nyote mnavyofahamu waziri wa ulinzi wa shirikisho Christine Lambrecht amemuomba Kansela amruhusu ajiuzulu.Kansela anauheshimu uwamuzi wa bibi Lambrecht na amemshukuru kwa kazi nzuri aliyoifanya katika nyakati hizi ngumu na za changamoto kama waziri wa ulinzi.Kansela atawasilisha pendekezo lake la atakayechukua nafasi hiyo kwa rais wa shirikisho katika muda mwafaka," alisema Hoffmann.
Shinikizo la kumpata waziri mpya wa ulinzi linaongezeka kutokana na ziara ya waziri wa ulinzi wa Marekani Loyd Austin anayetarajiwa kuwasili Berlin Alhamisi na atashiriki mkutano Ijumaa katika ya jeshi la Marekani mjini Ramstein kujadili suala la kuipatia msaada zaidi Ukraine.