1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSaudi Arabia

Saudia yasema mazungumzo ya Sudan kujadili usitishaji vita

Hawa Bihoga
29 Oktoba 2023

Saudi Arabia imesema Jumapili kwamba mazungumzo ya Jeddah kati ya pande zinazozozana nchini Sudan, yatazingatia makubaliano ya kusitisha mapigano na usambazaji wa misaada ya kiutu na si juu ya masuala mapana ya kisiasa

https://p.dw.com/p/4YAaa
Mazungumzo ya amani ya Sudan yamekuwa yakifanyika Saudia
Mazungumzo ya amani ya Sudan yamekuwa yakifanyika SaudiaPicha: AFP

Katika taarifa iliotolewa na wizara ya mambo ya nje, mazungumzo hayo yalioanza siku ya Alhamisi yananuwia kuwezesha uwasilishwaji wa misaada ya kiutu, hatua nyingine za kujenga amani na usitishwaji wa kudumu wa mapigano.

Soma pia: Jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF wako tayari kushiriki mazungumzo Jeddah

Majaribio ya awali ya upatanishi yaliosimamiwa na Marekani na Saudi Arabia yalifanikiwa kwa muda mfupi, lakini yalikiukwa. Hata hivyo Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa masuala ya kibinadamu Martin Griffiths amesema mazungumzo hayo hayakuanza mapema kama ilivyostahili, kutokana na hali ya kiutu nchini humo.

Tangu kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan takriban watu 9,000 wameuwawa na zaidi ya milioni 5.6 wakikimbia makazi yao.