Saudia na Qatar zapongeza utambuzi wa dola la Palestina
22 Mei 2024Saudi Arabia imekuwa ikiunga mkono hatua hiyo na kamwe haijawahi kuitambua Israel kama dola, japo mwezi Septemba mwanamfalme ambaye ndie mtawala wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman alisema hatua zimepigwa pamoja na Marekani, kuhusu makubaliano ya kuwa na uhusiano wa kidiplomasia, yanayoweza pia kuhusisha hatua ya kuimarisha usalama na masuala mengine
Qatar imesema imekaribisha uamuzi wa kuitambua Palestina kama dola huru, ikisema ni hatua muhimu kuelekea suluhu ya madola mawili.
Jordan na Baraza la ushirikiano la nchi za Ghuba GCC pia zimepongeza uamuzi huo zilizouita wa kihistoria, huku Ujerumani kupitia msemaji wake wa masuala ya nje ikisisitiza uwepo wa suluhu ya madola mawili lakini ikatahadharisha kua lazima kuwepo na mazungumzo kabla ya hilo kufanyika.