Saudi Arabia yasikitishwa na kutotambuliwa Palestina
19 Aprili 2024Siku ya Alhamisi (Aprili 18), Marekani ilitumia kura yake ya turufu kuzuia hatua hiyo kuchukuliwa, licha ya kuongezeka kwa sauti za ghadhabu katika jumuiya ya kimataifa juu ya mgogoro wa kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.
Soma zaidi: Marekani yatumia kura ya turufu kupinga azimio la Gaza
Nchi 12 ziliunga mkono muswaada huo wa azimio uliowasilishwa katika Baraza la Umoja wa Mataifa na Algeria huku Uingereza na Uswisi zikijizuia kupiga kura.
Ofisi ya Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Wapalestina iliitaja hatua ya Marekani kama uchokozi wa wazi unaousukuma zaidi Ukanda ya Mashariki ya Kati katika kiza.
Balozi wa Algeria katika Umoja wa Mataifa, Amar Bendjama, alisema kuungwa mkono kwa azimio hilo na wanachama wengi ni ujumbe tosha kwamba Wapalestina wanatambuliwa katika Umoja wa Mataifa.