1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Saudi Arabia yakosa kiti Baraza la Haki za Binaadamu UM

10 Oktoba 2024

Saudi Arabia imeshindwa kupata kiti kwenye Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa kufuatia kampeni ya makundi ya haki za binaadamu yanayolilaumu taifa hilo kwa uvunjajii mkubwa wa haki.

https://p.dw.com/p/4lbXZ
Salman bin Abdulaziz
Mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi ArabiaPicha: Andrew Caballero-Reynolds/REUTERS

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 193 hapo jana liliwachaguwa wajumbe wapya 18 kuingia kwenye Baraza la Haki za Binaadamu  lenye wajumbe 47, ambao hupatikana kwa mujibu wa maeneo ili kuhakikisha uwakilishi wa kijiografia.

Baraza hilo lililoundwa mwaka 2006 na lenye makao yake makuu mjini Geneva, Uswisi, huwa linatathmini rikodi za haki za binaadamu kwa nchi zote kila baada ya muda, kuteuwa wachunguzi huru na kutowa ripoti za matukio ya utesaji, mauaji  na upotezaji watu.

Soma zaidi: Saudi Arabia: Visa vya kunyongwa vyaongezeka licha ya ahadi za haki za binaadamu

Nchi zilizoingia kwenye Baraza hilo kutoka eneo la Asia na Pasifiki mwaka huu ni Thailand, Cyprus, Qatar, Korea Kusini na Visiwa vya Marshall.

Kabla ya kupigiwa kura, mkurugenzi wa shirika la Human Rights Watch, Louis Charbonneau, aliitaja Saudi Arabia kuwa haifai kuwamo kwenye Baraza la Haki za Binaadamu.