1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliochanja wanaruhisiwa kushiriki ibada ya Umrah Makka

8 Agosti 2021

Saudi Arabia itaanza kuwapokea wageni waliopata chanjo ya Covid-19 katika mji mtakatifu wa Kiislamu wa Makka kama sehemu ya ibada ya Umrah, ikiwa ni takribani miezi 18 baada kufungwa kutokana na kuzuka Covid-19

https://p.dw.com/p/3yhJr
Jährliche Hadsch-Wallfahrt in die heilige Stadt Mekka
Picha: Ahmed Yosri/REUTERS

Shirika la habari la Saudi limesema Wizara ya Hijja na Umrah imetangaza kuanza kupokea raia wa taifa hilo wenye nia ya kutaka kushiriki ibada ya Umrah, lakini pia kwa awamu watapokea maombi kutoka mataifa mbalimbali.

Aidha taarifa hio imeongeza kusema mamlaka zitaanza kukubali maombi ya kusafiri kuanzia kesho Jumatatu. Kwa hatua hiyo uwezo wa kupiokea wageni katika mji ya Makka na Madina utaongezeka na kufikia watu milioni 2, kutoka 60,000.

Ibada ya Umrah ambayo kwa kawaida inafanyika katika kipindi chochote cha mwaka, ilifunguliwa tena Oktoba kwa mahujaji wa ndani, baada ya kufungwa kabisa kutokana na mripuko wa janga la corona.

Janga la Covid-19 limevuruga ibada zote za mahujaji mjini Makka

Saudi-Arabien Mekka | Pilgerfahrt | Berg Arafat
Mahujaji wakiwa mjini MakkaPicha: Ahmed Yosri/REUTERS

Janga la virusi vya corona kwa kiasi kikubwa lilivuruga hija zote, ambazo kwa kwa kawaida ni chanzo muhimu cha mapato cha Saudi Arabia,  kwa pamoja zinaweza kuliingiza taifa hilo pato la takribani dola bilioni 12 kwa mwaka. Kabla ya uamuzi huu wa Jumapili, ni mahujaji walipata chanjo wa ndani ya taifa hilo tu, ndio walikuwa wanaruhusiwa kushiriki umrah, ingawa Híjja imekuwa ikifanyika kwa mahudhurio madogo sana tangu kuanza kwa janga hilo.

Ripoti ya shirika la habari la taifa hilo SPA, likimnukuu Naibu Waziri, Abdulfattah bin Sulaiman Mashat limeandika, hujaji yeyote lazima awe kapata chanjo yenye kutambuliwa na mamlaka ya taifa hilo na akubali kwenda karantini. Serikali ya Riyadh imekuwa ikitumia mabilioni ya fedha katika jaribio la kuijenga sekta ya utalii kuanzia chini kabisa, kama sehemu ya juhudi za kuwa toafuti na uchumi wake unaotegemea biashara ya mafuta.

Serikali imeongeza kasi ya kampeni ya chango ya kitaifa, ikiwa kama sehemu ya kufufua utalii na sekta nyingine ziliathiriwa na janga la covid-19 kama mashindano ya michezo na burudani kwa ujumla wake.

Chanjo ni lazima kwa kila mmoja anayetaka kuingia katika taasisi za serikali na za kibinafsi, zikiwemo taasisi za elimu, kumbi za burudani pamoja na usafiri wa umma. Hadi wakati huu Saudi Arabia imeorodhesha karibu watu 532,000 walioambukizwa virusi vya corona na zaidi ya watu 8,300 wameshakufa kutokana na Covid-19.

Vyanzo: AFP/RTR