1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Haki sawaSaudi Arabia

Saudi Arabia kuongoza kongamano la haki za wanawake

28 Machi 2024

Umoja wa Mataifa umeiteua Saudi Arabia kuongoza tume yake kuhusu hadhi ya wanawake, CSW kwa muda wa mwaka mmoja.

https://p.dw.com/p/4eEC7
Haki za wanawake nchini Saudi Arabia
Afisa wa polisi akimkabidhi maua mwanamke anayeendesha gari huko Jeddah, Saudi Arabia mnamo Juni 24, 2018. Saudi Arabia iliondoa marufuku ya wanawake kuendesha magari iliondolewa kama sehemu ya Mpango wa "Dira ya Saudi Arabia ya 2030".Picha: Yomiuri Shimbun/AP Images/picture alliance

Tume ya CSW yenye mataifa wanachama 45 ilimteua Balozi wa Saudi Arabia Abdulasis Alwasil bila kupigiwa kura mjini New York jana Jumatano, kuwa mwenyekit wa kikao kijacho, uamuzi ambao ulilishtua shirika la haki za binadamu la Amnesty International.

Saudi Arabia ni taifa la utawala wa Kifalme lililoshika nafasi ya 132 kati ya 146 katika ripoti ya usawa wa kijinsia ya Jukwaa la Kiuchumi la Dunia ya mwaka 2023.

Wakati wa kikao cha tume hiyo, mwenyekiti wa sasa kutoka Ufilipino alimuwasilisha balozi wa Saudi Arabia kama mgombea pekee.

Afisa wa Amnesty Natalie Wenger, ambaye majukumu yake katika tawi la shirika hilo nchini Sweden yanahusisha pia Saudi Arabia, alisema uteuzi huo umewashtua ingawa haukuwa mshangao, akitaja kampeni kubwa inayoendeshwa na mwanamfalme wa Saudi Mohammed bin Salman kutakasa sifa ya taifa hilo kuhusu suala la haki za binadamu na haki za wanawake.