1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudi Arabia na Iran zabadilishana mabalozi

Josephat Charo
6 Septemba 2023

Saudi Arabia na Iran zimebadilishana mabalozi baada ya kipindi cha miaka saba ya ukimya tangu mahusiano baina ya nchi hizo mbili yalipovurugika. Ubalozi wa Iran mjini Riyadh ulifunguliwa rasmi mnamo Juni mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4VzcZ
Saudi-Arabien Eröffnungszeremonie der iranischen Botschaft in Riad
Picha: Wang Haizhou/Xinhua/picture alliance

Saudi Arabia na Iran zimebadilishana mabalozimiaka saba tangu mahusiano baina ya nchi hizo mbili yalipovurugika. Balozi wa Saudi Arabia nchini Iran Abdullah Alanazi aliwasili jana Jumanne mjini Tehran kuanza majukumu yake.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Saudia balozi Alanazi alisema utawala wa Saudia Arabia unatambua umuhimu wa kuimarisha mahusiano, kuongeza ushirikiano na kuupeleka uhusiano kwenye upeo mpana zaidi. Alanazi alikuwa balozi wa Saudi Arabia nchini Oman.

Hapo jana pia balozi wa Iran nchini Saudi Arabia, Alireza Enayati, aliwasili mjini Riyadh ambako alilakiwa na maafisa wa ubalozi na wa wizara ya mambo ya nje. Enayati alikuwa balozi wa Iran nchini Kuwait.